Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John leo Tar. 9 Septemba 2023 amepokea vifaa vya michezo viliotolewa na Benki ya CRDB tawi la Kyerwa kwa ajili ya Timu za Kyerwa Veterans za Rubwera na Nkwenda kwa lengo la kuendelea kuboresha michezo na mahusiano mazuri na jamii.
Katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji amepokea jezi 18, viatu 18, mipira ya miguu minne, mipira ya wavu miwili, Bips Mazoezi 30 na koni za mazoezi 50.
Aidha Mkurugenzi ameishukuru Benki ya CRDB kwa ufadhali wa vifaa hivyo ambavyo vitaongeza tija katika maendeleo ya sekta ya michezo katika Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved