Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa leo tar. 26 Septemba 2023 wamefanya kikao kazi chenye lengo la kujadili na kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali zinawakabili wafanyakazi katika mazingira yao, ili kuboresha na kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Akiongoza kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John amewasisitiza watumishi wote kufanya kazi kwa bidii na kila mmoja kuonyesha uwezo wake katika kutekeleza majukumu yake.
“Ninaamini kila mmoja anaweza kufanyakazi, kila mmoja afanye kazi yake ambavyo anaweza kuifaya kadri ya uwezo wake, tutimize majukumu yetu.” amesema Mkurugenzi.
Aidha amewataka watumishi kutunza siri za ofisi, kuheshimu nyaraka za serikali na kufuata taratibu na sheria zilizowekwa kuwaongoza watumishi wa umma ili waweza kufanya kazi kwa uadilifu na uwajibikaji.
Vile vile amewasihi watumishi kuwa na upendo na umoja ambao utajenga timu ambayo itaweza kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo mmoja.
Kwa upande wa watumishi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali ikiwemo ya madeni yao, kufanya kazi katika masaa ya ziada na siku za mapumziko, uhaba wa usafiri na kupatiwa majibu na ufafanunuzi wa maswali yao.
Aidha wengine wametoa maoni na ushauri wa namna ya kuboresha utendaji kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa uongozi wake uliopelekea halmashauri kupata tuzo ya utendaji wa kazi na kutoa huduma kwa wananchi kwa mwaka 2022/2023 katika Mkoa wa Kagera.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved