Mkuu wa ya Kyerwa Mhe. Zaituni Abdallah Msofe ametoa futari Kwa waumini wa kiislamu na wananchi wote.Katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, taasisi na viongozi wa dini kwa nyakati tofauti wametoa shukrani na pongezi Kwa tendo hilo jema.
Mhe.Zaituni Abdallah Msofe amesema ninawaomba ndugu zangu tulinde Amani na utulivu maana ni jukumu letu kulinda Amani hususani wakati huu tunapoelekea kuelekea kwenye maadhimisho ya sikukuu ya IDD. Pia amewaomba Wazazi kusimamia Malezi kwa Vijana na kuwaelekeza watoto kufuata Mila na destuli za Nchi yetu. Pia amewaomba Viongozi kuendelea kuwajali Yatima,Wajane na watu wasiojiweza.
Mwisho amewashukuru na kuwaombea baraka na heri za Mwenyezi Mungu huku akiwaomba waendelee kumwombea Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan
Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Kyerwa Sheikh Banoba kwa niaba ya waislamu wote amemshukuru na kumpongeza Mkuu wa ya Kyerwa kwa tendo hilo la kiungwana pia amehimiza Amani kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya Eidd Alfitri.
Chanzo: Flavius Kabalila
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved