Kikao cha Tathimini ya Mkataba wa lishe kimefanyika leo Tar. 21 Novemba 2023 katika ukumbi wa Rweru Plaza kikiwa na lengo la kupokea na kujadili tarifa ya utekelezaji wa mkataba huo katika Wilaya ya Kyerwa kwa robo ya Kwanza ya kuanzia mwezi Julai hadi Septemba Mwaka 2023/2024.
Akiongoza kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka wajumbe wa kamati ya Lishe kuongeza juhudi ili kutokemeza matatizo yatokanayo na ukosefu wa lishe bora.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha robo ya mwaka Bi. Irene Cleophace amesema kunaongezeko la 2% la wanafunzi wanaopata walau mlo mmoja shuleni huku kukiwa na changamoto ya viwanda vikubwa na vidogo vya vinavyorutubisha unga wa mahindi na idadi ndogo ya shule zinazotumia unga huo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved