Maadhimisho ya siku ya Lishe kitaifa pamoja na uzinduzi wa kampeni ya lishe kwa vijana balehe katika Wilaya ya Kyerwa yamefanyika tarehe 30 Oktoba 2023 katika Kijiji cha Muhulire Kata ya Nkwenda.
akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewahimiza wazazi na walezi kuimarisha malezi kwa Vijana balehe ili waweze kuwa na maamuzi sahihi na kujiepusha na tabia zisizofaa katika jamii kwani katika umri huo vijana wengi ndio hujiingiza katika makundi yasiyofaa.
Aidha amewataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu na kuimarisha lishe kwa watoto wa shule kwani hilo ni jukumu lao, ikiwa ni pamoja na kuanzisha bustani za mbogamboga katika shule ili ziweze kutumiwa na wanafunzi katika kuboresha afya zao.
“Swala la Mbogamboga bado ni tatizo, watoto kweli wanakunywa uji lakini bado tunahitaji mbogamboga na matunda. Kyerwa inaardhi ya kutosha na shule nyingi zinaardhi za kutosha tujitahidi kuwa na programu ya kupanda mbogamboga ambazo zitatumiwa na wanafunzi kuboresha lishe zao.” Ameeleza Mhe. Msofe.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Wilaya ya Kyerwa, Bi. Arene Cleophace amesema vijana balehe ni kundi la watu ambao linamabadiliko mengi na linaitaji lishe iliyobora na pia ni kundi ambalo linatabia hasi za ulaji wa chakula kwa kufuata mkumbo ambao hupelekea kupata maradhi yasiyoambukizwa.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya, “Lishe bora kwa vijana Balehe, Chachu ya Mafanikio yao” Kauli hii imepewa kipaumbele kwa Vijana kuelimishwa kuwa lishe bora husaidia kujenga mwili, kulinda mwili na husaidia kumuandaa kijana kuwa mzazi bora kwa kuimarisha afya na mifumo ya uzazi.
shughuli mbalimbali zimefanyika katika maadhimisho hayo ikiwemo; kutoa elimu ya lishe, mapishi kwa vitendo, tathmini ya hali ya lishe pamoja na kupanda miti ya matunda.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved