Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe Oktoba 30, 2023 amefanya mkutano na Wananchi katika Kata ya Kamuli ikiwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero zao.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliambatana na Katibu Tawala wa Wilaya, wataalamu mbalimbali kutoka TARURA, RUWASA, NIDA, Viongozi wa Ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu kutoka halimashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Miongoni mwa kero kubwa zilizoibuliwa na wananchi ni ukosefu wa vitambulisho vya NIDA, suala ambalo limeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa na wataalamu kutoka ofisi ya NIDA ambao walitumia nafasi hiyo kumpa Mhe. Mkuu wa Wilaya kadi 313 za Vitambulisho vya NIDA ili azigawe huku kukiwa na nyingine zaidi 700 ambazo zimepelekwa ofisi ya Mtendaji wa Kata ila wanachi hawakuwa na taarifa ya kwenda kuzichukua na kuwataka wakazichukue.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi ambao hawajafanikiwa kupata Vitambulisho vyao wafuate taratibu ili waweze kupatiwa vitambulisho hivyo huku akihimiza wataalamu kuendelea kutoa elimu ya namna ya kupata Vitambulisho vyao.
Vile vile amewataka viongozi ngazi Kitongoji, Vijiji na Kata kufanya mikutano na wanchi mara kwa mara ili kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi.
Pia amekemea wananchi wanaouza kahawa ikiwa bado iko shambani jambo ambalo hupelekea kuuza kwa bei ndogo na kusababisha serikali kukosa mapato kwa kufanya biashara ya magendo ya kuuza kahawa nje ya nchi kinyume na taratibu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved