DESEMBA 06, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Zaituni Msofe ameongoza Kikao Cha tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Mhe. Msofe ametoa shukrani kwa Viongozi wa vyama vya siasa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, wanakamati, wananchi, taasisi binafsi na za Serikali na watumishi wote kwa ushirikiano wao waliounesha toka wakati wa maandalizi hadi kukamilika kwa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Kyerwa.
Aidha ametoa tuzo kwa baadhi ya Watumishi na Wadau waliofanya vizuri na kusema kuwa "Tumetoa tuzo ili kutoa morali na motisha kwa watu ili waendelee kufanyakazi zaidi"
Awali Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Kyerwa, Ndg. Daima Nkinda ametoa taarifa kuwa Wilaya ya Kyerwa imepata alama 80.43 na imeshika nafasi ya 4 Kimkoa, Nafasi ya 5 Kikanda na nafasi ya 16 kitaifa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved