MKUU wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe leo tarehe 19 Julai 2023 ametembelea mradi wa maji wa Runyinya Chanya katika kata ya Nkwenda, unaotekelezwa na Mkandarasi wa JAMTA Costruction Investiment Ltd Vumwe Jeneral Service and Supplies Co. Ltd na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.
Mradi huo ulitakiwa kukamilika na kuanza kuhudumia wananchi wa kata tatu za Nkwenda, Rwabwere na Iteera Juni 30 mwaka huu umeonekana kusuasua na Mkandarasasi kuomba kuongezewa muda wa miezi mitatu ili kukamisha mradi huo wenye thamani ya shilingi 4,628,169,052.50.
“Tunawaangusha wananchi wanaotegemea kupata maji kupitia mradi huu, tunaiangusha serikali kwa kuchelewesha miradi hii ambayo inatoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Ongezeni kasi kwa kipindi hichi kilichobaki kwani sitarajii kuona mkiomba kuongezewa muda tena.” Amesisitiza Mhe. Msofe.
Naye Mhadisi wa RUWASA Wilaya ya Kyerwa Eng. Shukrani Tungaraza amesema mkandarasi huyo alilipwa stahiki zake mapema na alitakiwa kukamisha mradi huo kwa wakati, waliamua kumuongezea muda wa miezi mitatu na kumtaka mkandarasi huyo kuheshimu mkataba pamoja na kuandika barua ya kuahidi kumaliza kazi kwa muda alioongezewa.
Kwa upande wake Mkandarasi wa mradi huo Eng. Kundaeli Mtangavo amesema atajitahidi kumaliza mradi huo kwa wakati kwani alipata changamoto ya kucheleweshewa mabomba makubwa ambayo yatafika wiki ijayo na kazi kendelea.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved