Katika mwendelezo wa kutembelea na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe, Novemba 1, 2023 amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Migina kata ya Songambele katika Wilaya ya Kyerwa.
Pamoja na kusikiliza kero za wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa amewataka wananchi wa Kata hiyo kutunza miundombinu ya barabara kwa kuacha kupitisha magari ya mizigo yenye uzito makubwa ambayo uzidi tani kumi kwani magari hayo huharibu barabara na kuvunja makaravati na kusababisha barabara hizo kutopitika na kusababisha kero kwa wananchi.
Amesema kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wa miundombinu hiyo na akiona magari yenye uzito mkubwa atoe taarifa sehemu husika ili hatua stahiki zichukuliwe na miundobinu hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kusaidia wananchi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Kyerwa amegawa vitambulisho vya NIDA 2,333 kwa wananchi wa Kata ya Songambele ambavyo vimekamilika na kuwasihi wale ambao hawakujiandikisha, wakajiandishe ili wapate vitambulisho vyao kwani zoezi hilo ni endelevu na linafanywa na Serikali bila malipo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico amewataka Viongozi wa Serikali ya Kijiji kusimamia na kutunza ardhi za vijiji na kuwazuia wananchi wa kata hiyo kuvamia ardhi za Kijiji na maeneo ya mabonde na milima kwani maeneo hayo ni mali ya Serikali ya Kijiji na mwanachi hatakiwi kuyavamia kiholela.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kyerwa SACF. James John amewataka wananchi kuanzisha ujenzi wa Zahanati katika Vijiji vyao ili vikifikia usawa wa maboma serikali itamalizia hatua zinazobaki huku kuwapa taarifa njema kuwa Shule mpya ya Masingi ya Chanyangabwa imesajiliwa na hivyo kuwasihi wazazi kuwaandikisha watoto wao na kwenda kusoma katika Shule hiyo.
Katika ziara ya hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa aliambatana na Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, Viongozi wa Ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu kutoka Halimashauri ya Wilaya ya Kyerwa, TARURA, RUWASA, NIDA na TANESCO.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved