MKUU wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe tarehe 29 Mei 2025 amefungua mafunzo ya awali ya jeshi la akiba kata ya Kyerwa Wilaya ya Kyerwa.
Akizugumza katika hafla hiyo amewapongeza vijana waliojitokeza na kuwasihi kuwa waone hiyo ni fursa ambayo itawafungulia njia itakayowasidia katika maisha yao endapo wataitumia vizuri.
“Vijana mliojitokeza katika mafunzo haya naamini mafunzo yatakapokamilika mtaenda kupata fursa mbalimbali, mafunzo haya yanahitaji uzalendo na uadilifu muende mkawe wazalendo na waadilifu. Msiende kuyatumia mafunzo vibaya.” Amewaasa Mhe. Msofe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved