MKUU wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe leo tarehe 20 Julai 2023 amefungua mafunzo ya awali ya jeshi la akiba kata ya Kikukuru Wilayani Kyerwa.
Akizugumza katika hafla hiyo amewapongeza vijana waliojitokeza na kuwasihi kuwa waone hiyo ni fursa ambayo itawafungulia njia itakayowasidia katika maisha yao endapo wataitumia vizuri.
“Vijana mliojitokeza katika mafunzo haya naamini mafunzo yatakapokamilika mtaenda kupata fursa mbalimbali, mafunzo haya yanahitaji uzalendo na uadilifu muende mkawe waazalendo na waadilifu. Msiende kuyatumia mafunzo vibaya.” Amewaasa Mhe. Msofe.
Awali Meja AD Ndelwa akitoa taarifa ya mafunzo hayo, amesema kuwa Mafunzo hayo yatatolewa kwa vijana 72 ikiwa ni wanaume 70 na wa kike wawili kutoka katika vijiji vyote vya kata ya Kikukuru na vijiji vya kata jirani ya Kitwe.
“Mafunzo haya yatatolewa kwa muda wa majuma 16 ambapo vijana watafundishwa kwata, usomaji wa ramani, mbinu za kivita, utimamu wa mwili, silaha ndogo, huduma ya kwanza, uhandisi wa medani na ujasiriamali ambao utawajengea uwezo wa kujiajiri ama kuajiriwa sehemu mbalimbali.”Alisema Meja Ndelwa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kikukuru Mhe. Tiiku Justus ameishukuru serikali kwa mpango wa kutoa mafunzo hayo kwa vijana katika kata ya Kikukuru na ameahidi kutoa ushirikiano katika kusimamia mafunzo hayo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved