"Mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF) iliyobereshwa umelenga kuhudumia kaya maskini na zilizo katika sekta isiyo rasmi" .Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa,Dokta Diocles Ngaiza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa maafisa waandikishaji 99 katika ukumbi wa Schostentant Isingiro hivi karibuni.
Mafunzo hayo yaliyofadhiriwa na mradi wa TUIMARISHE AFYA, yamelenga kupanua uelewa kwa maafisa waandikishaji kutoka Vijiji 99 vya Wilaya ya Kyerwa.Aidha CHF iliyoboreshwa inawigo mpana wa matibabu ambapo kaya yenye wanafamilia 6, italipia shilingi elfu thelathini tu (30,000/=) na kuweza kupata huduma za matibabu kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali za rufaa za mikoa.Aidha makundi ya wanufaika ni kaya zinazotokana na wanafunzi, familia, taasisi ,na bodaboda.Pia kila mwananchama atapatiwa kitambulisho chake cha uanachama tofauti na CHF iliyopita ambapo kaya moja ya watu sita ilitumia kitambulisho kimoja.
Aidha, waandikishaji hao walipatiwa elimu juu ya usajili wa wananchama kwa kutumia simu za kupangusa(smart phones) .
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved