Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Shaban I. Lissu amezindua chanjo dhidi ya kansa ya kizazi hivi karibuni, kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 14 katika zahanati ya Kaisho.
“HPV” ni chanjo dhidi ya virusi vya HPV vinavyosababisha saratani ya mlango wa kizazi.Chanjo hii inawakinga wasichana wenye umri wa miaka 14 dhidi ya maradhi haya.
Aidha,chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi hutolewa mara mbili ili kupata kinga kamili, baada ya kupata chanjo ya kwanza.Chanjo ya pili hutolewa baada ya miezi sita kupita.
Wilaya ya Kyerwa imezindua chanjo hii kiwilaya tarehe 23 Aprili, 2018. Jumla ya wasichana 3,271 wameorodheshwa, kutoka shuleni ni wasichana 2,745 na wasichana 526 kutoka ngazi ya jamii .
Aidha mpaka taarifa hii inaenda hewani jumla ya wasichana 842 kutoka shule mbalimbali Wilayani wameshapatiwa chanjo hii,huku wasichana 11 kutoka katika jamii nao wamepatiwa huduma hii.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved