Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kyerwa leo tar. 17 Julai 2023 imepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025 kwa kipindi cha Januari hadi Juni, mwaka huu katika ukumbi wa CCM Wilayani Kyerwa.
Akiwasilisha taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika wilaya ya Kyerwa.
Mhe. Msofe amesema, “Miradi ya ujenzi wa miundombinu kama inavyoelekezwa na serikali kupitia idara na vitengo mbalimbali za elimu (sekondari na msingi), afya, kilimo, mifugo na uvuvi, utumishi na utawala, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, tehama, maji, umeme na barabara.”
Aliongeza kwa kusema kuwa mapungufu yaliyojitokeza katika utekelezaji wa ilani ya chama katika baadhi ya miradi yamepokelewa na yatafanyiwa kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kyerwa Mhe. Daniel Damiani amesema wameridhishwa na utekelezaji wa miradi na kumpongeza mkuu wa wilaya, mkurugenzi mtendaji, mwenyekiti wa halmashauri pamoja na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuendelea kuijenga wilaya.
“Kazi nzuri imefanyika, mapungufu ni ya kibinadamu, tunawapenda watumishi wa wilaya na tutatoa ushirikiano. Na nawaagiza vingozi wa kata CCM washiriki katika kusimamia miradi na kama kunachangamoto zifikishwe ofisini mapema.”
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved