Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya masuala ya fedha, utunzaji wa fedha na huduma ndogo za kifedha, yaliyotolewa leo tarehe 11 Februari 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Akiongoza Mafunzo hayo, Meneja Fedha na Utawala wa BoT Tawi la Mwanza Ndg. Meso Gaitoti amesema kuwa Benki kuu ya Tanzania inatambua kuwa suala la fedha ni nyeti hivyo ni vyema elimu ikatolewa kwa makundi mbalimbali ili kuwajengea uelewa wa fedha.
Ndg. Meso amesema, kutambua alama na usalama wa fedha, Utunzaji wa fedha, fursa za uwekezaji, ubadilishwaji wa fedha kwenye mzunguko, uingizwaji wa fedha za kigeni na huduma ndogo za kifedha, ni muhimu kupatiwa elimu ili kuweza kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa SACF. James John amewashukuru wawezeshaji kutoka BoT kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka waliohudhuria mafunzo hayo kuyazingatia na kuyafanyia kazi pamoja na kuwafikishia ujumbe wengine ili mafunzo hayo yaweze kuwa na tija kwa jamii ya Kyerwa.
Wawakilishi wa makundi ya wadau ambao walihudhuria mafunzo hayo ni Wafanyabiashara, wavuvi, Wawekezaji, Wastaafu, Watumishi, Viongozi wa Vyama vya Ushirika, Watoa huduma ndogo za kifedha na viongozi wa vyama vya SACOSS katika Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved