Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imepokea jumla ya shilingi 1,700,000,000.00 kupitia programu ya UVIKO-19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 85 vya madarasa katika shule 23 za sekondari za Serikali.
Kwa ujumla ujenzi wa miundo mbinu umefikia asilimia 52. Aidha, kwa mujibu wa taarifa za kifedha kwa kutumia mfumo wa taarifa ngazi ya vituo (FFARS), mpaka tarehe 25 Novemba, 2021,
jumla ya kiasi cha shilingi 578,107,525.45 kimeshalipwa kwa kazi za ufundi na manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu katika shule hapa Wilayani.
Mpaka sasa, jumla ya vyumba vya madarasa 18 ujenzi umefikia hatua ya lenta, madarasa 32 yapo hatua ya hanamu, madarasa 21 yapo hatua ya kupandisha kenchi, madarasa 3 yapo hatua ya uezekaji,
na madarasa 11 yapo hatua ya umaliziaji.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved