Wilaya ya Kyerwa kwa kipindi cha mwezi Disemba, 2022 mpaka Januari, 2023 imezindua vituo 4 vya kutolea huduma za Afya Wilayani hapa vilivyogharimu kiasi cha shilingi 1,224,685,000. Vituo hivi ni kituo cha Afya Rutunguru,Mabira, Zahanati ya Iteera, na Zahanati ya Rwabwere.
Miradi hii imetekelezwa kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato iliwa ni pamoja na fedha za Tozo ya Miala ya simu (Serikali kuu), Fedha za Mfuko wa Jimbo, Halmashauri kupitia Mapato ya Ndani, na Nguvu za Wananchi.
Zahanati ya Chanya imejengwa na kuzinduliwa mnamo tarehe 13 Disemba, 2022 ikiwa itahudumia wakazi zaidi ya 5000 wa kijiji cha Chanya na maeneo jirani. Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi 112,440,000.Zahanati hii ilianza kujengwa mwaka 2008 kupitia michango ya wananchi na baadae Serikali iliwaunga nguvu wananchi.
Zahanati ya Iteera nayo imezinduliwa tarehe 13 Disemba, 2022 ikiwa imetumia jumla ya kiasi cha shilingi 112,245,000 ikiwa imelenga kuwahudumia jumla ya wakazi 6000 wa kijiji cha Chanya na maeneo jirani.Aidha, Zahanati hii ilianza kujengwa kuanzia mwaka 2019.
Kituo cha Afya Rutunguru kimezinduliwa tarehe 30 Disemba, 2022 na kimegharimu kiasi cha shilingi 500,000,000 fedha za tozo kutoka Serikali kuu.Kituo hiki kilianza kujengwa kuanzia oktoba, 2021 na kinatarajiwa kuwahudumia jumla ya wakazi 20,000 kutoka kata za Rutunguru na vijiji jirani.
Aidha, kituo cha Afya cha Mabira kimezinduliwa mnamo tarehe 4 Januari, 2023 kikilenga kuwahudumia wakazi wa Mabira na kata jirani wapatao 30,000.Kituo hiki kilianza kujengwa mnamo Disemba, 2021 na kimegharimu kiasi cha shilingi 500,000,000 fedha kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizindua miradi hii kwa nyakati tofauti tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mheshimiwa Rashid Mwaimu alimshukuru Mheshimiwa Rais, Dokta Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani Kyerwa, na kuwasihi watumishi kufuata maadili katika kuhudumia jamii. Aidha, aliusisitiza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha madawa na vifaa tiba vinapatikana katika vituo vya Afya ili kuondoa kero wananchi kwenda kutafuta dawa katika vituo binafsi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved