Shirika la MEDA, na IITA kwa kushirikiana na chuo cha utafiti cha Ukiriguru wameendesha warsha ya siku moja, kwa waheshimiwa madiwani juu ya uzalishaji wa mbegu bora za mihogo katika ukumbi wa ELCT Kyerwa leo tarehe 2 May, 2018 .Warsha hii ambayo imelenga kubaini na kutatua changamoto za uzalishaji wa mbegu za Muhogo kibiashara ,imewashirikisha pia baadhi ya wakulima wa zao la muhogo hapa Wilayani ili kupata picha halisia katika jamii.
Akifungua mafunzo hayo,mgeni rasmi mheshimiwa Singsbert Kashunju diwani wa kata ya Rukulaijo na mwenyekiti wa Halmashauri amesema ” muhogo huu tutakao upanda hapa Wilayani utakuwa suluhisho la matatizo yetu kwa mazao kama ndizi yaliyoshambuliwa na ugonjwa wa unyanjano,hivyo huu utakuwa ni mbadala wa chakula kwa wananchi wetu”.
Aidha mwezeshaji toka MEDA(Shirika la Kimataifa lenye malengo ya kuondoa umaskini kwa njia ya kibiashara), ndugu Everlyn Peter amefafanua kwa wajumbe utaratibu wa kupata mbegu za muhogo na vigezo vinavyotakiwa kwa wakulima wajasiliamali wazalishaji wa mbegu bora za muhogo wanavyohitajika kuwa navyo.Hii ni pamoja na kuwa na rasilimali fedha,umbali kati ya shamba na barabara,usajili na ukaguzi wa shamba,uwepo wa ardhi ya kutosha na fursa za umwagiliaji.
Mradi huu wa BEST CASSAVA umeanza mwaka 2017 na utaisha 2021 na unafadhiliwa na taasisi ya Bill & Merinda gate Foundation.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved