Uzinduzi na utoaji wa mikopo ya wajasiriamali kanda ya ziwa ulifanyika tarehe 4 Novemba,2017 mkoani Geita.Mheshimiwa Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu ,sera,bunge,ajira ,vijana na watu wenye ulemavu Jenesta Mhagama(Mb) alikuwa mgeni rasmi.Wilaya ya kyerwa tulikuwa na vikundi 7 vimepita kwenye assessment na vimepatiwa mikopo yenye jumla ya Tsh,169,740,000 kutoka baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi-NEEC chini ya mfuko wake wa Mwananchi Empowerment Fund(MEF) kupitia Benki ya Posta Tanzania(TPB) NA mfuko wa UTT Microfinance huku msimamizi mkuu ni FERUSCO VIKOBA.
Orodha ya vikundi vilivyopata mkopo sambamba na fedha ni vikoba Mabira (Tsh.9,690,000),vikoba Amka(Tsh.4,080,000),vikoba Nkwenda(Tsh 15,000,000),vikoba Rugarama(Tsh 4,920,000),vikoba Murile(Tsh 70.000,000),vikoba Omukishanda "C" (Tsh 18,750,000), na vikoba Omukishanda "A" (Tsh 46,800,000)
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved