Wajumbe Baraza la Wafanyakazi Wilaya ya Kyerwa wamefanya kikao cha baraza leo tarehe 13 Oktoba 2023 ili kujadili masuala ya utawala bora na usimamizi wa rasilimali watu katika ukumbi wa Rweru Plaza Wilayani Kyerwa.
Akiongoza kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mwl. Mayala Sengerema amesema Halmashauri inathamini mchango wa watumishi na kushughulikia changamoto zinazowakabili ili waweze kupata stahiki zao ipasavyo.
Akiwasilisha taarifa ya Idara ya Utawala na Utumishi, Bw. Frances Mwita amesema idara imeshughulikia kero mbalimbali za wafanyakazi zikiwemo za kuwapandisha vyeo na madaraja, malipo ya stahiki za watumishi, kulipa madeni, kuthibishwa kazini, kuwaruhusu kujiendeleza na masomo, kutoa motisha kwa wafanyakazi bora na kuajiri watumishi wapya wa kada mbalimbali ili kuleta ufanisi katika mazingira ya kazi Wilayani Kyerwa.
Kwa upande wao wajumbe wa baraza la wafanyakazi wameishauri idara ya Utawala na Utumishi masuala mbalimbali ikiwemo kushughulikia kero za madeni ya baadhi ya wafanyakazi na kufuatilia ulipaji wa michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ili wakifikia umri wa kustaafu wasije kuhangaika.
Pia wajumbe wamemuidhinisha Bw. Riziki Obedi kuwa Katibu Msaidizi wa muda wa baraza la wafanyakazi la Wilaya ya Kyerwa ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi baada ya katibu msadizi wa baraza hilo kuhamia sehemu nyingine.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved