Baraza la Madiwani la Kwanza kwa 2020-2025 wilayani Kyerwa limefanyika tarehe 03.12.2020 kwa kuongozwa na Mwenyekiti wa muda Ndg, S.I Benjamin Mwikasyege (Aliyesimama pichani) ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyerwa. Mwenyekiti huyo wa muda ni kwa mujibu wa Sheria za uendeshaji wa Serikali za Mitaa pale Mwenyekiti wa Halmashauri anapokuwa hajachaguliwa. Mwenyekiti huyo wa muda aliongoza uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Makamu wake ambapo Mhe, Bahati Heneriko Lekayo (Diwani wa Kata ya Rwabwere) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Mhe, Clarence Rugemalira Rugimbana (Diwani wa Kata ya Mabira) alichaguliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti. Aidha baada ya Mwenyekiti kuchaguliwa alikabidhiwa kiti na kuendelea kuendesha kikao hcho cha Baraza kwa kuunda Kamati zote za kudumu kwa kuteua Wajumbe wa Kamati hizo. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Wakuu wa Idara, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi waliofanikiwa kufika. Mwenyekiti aliyechaguliwa alitumia fursa hiyo kueleza mwelekeo wa Halmashauri baada ya Uchaguzi kukamilika ambapo alisisitiza kuepuka makundi ya kisiasa ambayo yanaweza kukwamisha maendeleo ya Halmashauri na pia alisisitiza kila mmoja katika Halmashauri kushiriki kikamilifu katika kukusanya na kusimamia na hatimaye kutumia mapato ya Halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Halmashauri. Aliwashukuru Watumishi na Viongozi wote katika ukumbi huo na kuomba ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved