Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, kwa pamoja wamepitisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya kiasi cha shilingi 30,248,943,791.77
Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 20 Januari, 2019 katika ukumbi wa E.L.C.T Kyerwa,Mwenyekiti wa Halmashauri (diwani wa kata ya Rukulaijo) mheshimiwa Singsbert Kashunju aliwashukuru mashirika na taasisi binafsi kwa ushirikiano wao na Halmashauri katika kuchangia utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha,naye Mgeni rasmi katika kikao hicho Mheshimiwa Rashid M.Mwaimu ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa,kwa niaba ya Serikali aliwasisitiza waheshimiwa madiwani kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kushiriki katika kuchangia utekelezaji wa bajeti .
Akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji,Afisa Mipango ,ndugu Innocent Maduhu alifafanua mchanganuo huo kuwa kiasi cha Tsh.16,954,701,599.00 kimetengwa kwa ajili ya mishahara ya watumishi, Tsh 2,043,090,500.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida(OC),Tsh 567,796,200 kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2019,Tsh 2,571,302,540.72 kwa ajili miradi ya maendeleo,Tsh 4,547,344,000.00 fedha toka wadau wa maendeleo,Tsh 2,406,208,952.00 fedha ya matumizi kwa mapato ya ndani,Tsh 605,000,000.00 fedha zitokanazo na michango ya Wananchi,Tsh 231,500,000.00 fedha zitokanazo na makusanyo ya CHF,Tsh 52,000,000.00 fedha zitokanazo na NHIF,na Tsh 270,000,000 fedha zitokanazo na malipo ya papo kwa papo.
Baraza la madiwani ,kwa pamoja baada ya majadiliano ya kina limeidhinisha jumla ya shilingi 30,248,943,791.77 kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved