Usafi wa mazingira wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi umefanywa katika Stendi ya Zamani ya Nkwenda pamoja na barabara zinazozunguka eneo hilo, leo tarehe 27 Januari 2024 katika Kata ya Nkwenda Wilaya ya Kyerwa.
Akizungumza na washiriki wa zoezi la usafi baada ya kumaliza zoezi hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Mwl. Stephano Ndabazi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa amewashukuru Viongozi, Watumishi, Wafanyabiashara na Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka kuendelea na utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Aidha amewataka viongozi wa Kata ya Nkwenda na Wilaya nzima kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwapiga faini wale ambao watakaidi kufanya usafi katika maeneo yao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved