Shirikisho la Mageuzi ya Kijani Afrika (AGRA) limetoa mafunzo ya kilimo kwa vijana na wanawake leo tar. 22 Agosti 2023 katika ukumbi wa vijana wa kanisa la KKKT Kata ya Nkwenda Wilaya ya Kyerwa yenye lengo la kuwaongezea tija wakulima katika mazao ya kilimo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Baraka Joshua amesema wanatoa elimu ya kuwawezesha vijana na wanawake tisini (90) kutoka katika vijiji vya Rukuraijo, Itera, Mgorogo na Muleba ambao baada ya mafunzo hayo ya siku moja wataenda kuwafundisha vijana wengine ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashamba darasa katika maeneo yao ili kuwasaidia vijana wengi zaidi na kuwainua kiuchumi.
Aidha amesema mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia wakulima katika kuongeza tija kwa kuwapatia ujuzi katika uzajilishaji wa mazao kwa kufuata kanuni na taraibu za kilimo cha kisasa na kutambua fursa za masoko ya mazao yao.
Katika mafunzo hayo shirika limelenga kutoa ujuzi kwa wakulima katika mazao ya Mahindi, Maharage na Mhogo kwani ni mazao ambayo yanastawi vizuri katika ukanda wa mikoa ya Magharibi mwa Tanzania ikiwemo Kagera, Kigoma, Katavi na Rukwa ambayo wameanza kutoa mafunzo hayo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved