Sekta ya uvuvi ni mojawapo ya sekta muhimu inayowapatia kipato, lishe pamoja na ajira wananchi wa wilaya ya Kyerwa.
Ukusanyaji wa takwimu za Uvunaji wa mazao ya Uvuvi.
Shughuli za Uvunaji wa mazao ya Uvuvi katika Wilaya ya Kyerwa zinafanyika katika maziwa madogomadogo 7 (Sattelite lakes), mabwawa,matingatinga (wetlands) pamoja na mto Kagera. Samaki wanaovuliwa ni Sato (Tilapia), Kamongo (Lungfish) na Kambare (Catfish).Uvuvi unaofanyika ni endelevu ili kuwa na faida kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo. Inakadiriwa takribani tani 82.8 za samaki zilivuliwa kwa mwaka 2014/2015 na 22.1. kwa mwaka 2015/2016 (Julai-Desemba)
Ufugaji wa samaki.
Ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa lishe hasa Protini, Kipato duni na ukosefu wa ajira, baadhi ya Wananchi wilayani wanajishughulisha na ufugaji wa Samaki katika Mabwawa ya kuchimba ambayo yameongezeka toka 42 mwaka 2014/2015 hadi 48 mwaka 2015/2016. Aidha ili kukabiliana na uvuvi haramu doria za mara kwa mara zinafanyika.
Udhibiti wa uvuvi haramu.
Ili kukabiliana uvuvi haramu doria za mara kwa mara zinafanyika.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved