Katika Wilaya ya Kyerwa shughuli ya kilimo inawawezesha wakazi zaidi ya asilimia 85 kujipatia chakula na kipato ambapo huzalisha mazao ya chakula ambayo ni ndizi,maharage, mahindi,ulezi, karanga, njegere,muhogo,viazi na mazao ya biashara ni kahawa na mtama. Wilaya inajitoshereza kwa chakula na ziada inauzwa kwenda kwenye masoko ya Wilaya nyingine na Nchi jirani. Jumla ya eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 253,215, hadi sasa jumla ya hekta 77,968 ambayo ni asilimia thelathini (30%) tu ya ardhi inayofaa kwa kilimo imelimwa. Asilimia tisini na nane (98%) ya eneo lote linalolimwa ni kwa kutumia jembe la mkono na asilimia mbili (2%) hutumia trekta.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved