Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa kushirikiana na Shirika la afya la MDH,inatarajia kuanza kampeni ya kufanya tohara kwa wanaume wote katika Wilaya ya Kyerwa .Zoezi hili litaanzia ukanda wa Nkwenda katika vituovya tiba vifuatavyo:Nkwenda,Songambele,Rwabwele,Rukulaijo, na Kitwechenkura.Baadae litaendelea katika ukanda wa Kaisho,Murongo hadi Mabira.
Kampeni hii itafanyika kwa takribani mwezi mmoja na huduma hii ni bure .Kwa yeyote anayetaka huduma hii anakaribishwa lakini unaombwa kusambaza ujumbe kwa wengine.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved