Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa leo imekabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo Duniani kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini. Miradi hii ni ya ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa ambavyo vimejengwa katika ubora na kwa viwango vinavyoweza kuhimili Tetemeko la Ardhi kwa gharama ya jumla ya Sh.279,406,000 mpaka kukamilika. Shule zilizonufaika na mradi huu ni Shule za Msingi za Nyakatuntu, Kikukuru, Masheshe na Nyamiyaga. Vyumba hivyo vya madarasa vimekemilika kwa 100% na vinatarajiwa kukabidhiwa kwa Wananchi mwishoni mwa mwezi Septemba, 2020. Halmashauri imetoa shukurani zake kwa Mfadhili ikiwa ni hatua zilizochukuliwa katika urejeshaji wa hali ya uharibifu wa miundombinu kufuatia Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016. Pichani mwenye kofia ni Msimamizi wa Mradi kutoka Ofisi ya UNDP Ndugu, Abbas Kitogo akipokea Taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyamiyaga aliyekabidhi taarifa hiyo kwa niaba ya wenzake.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved