Milioni moja na laki mbili (1,200,000) zatolewa rambirambi, Wakazi wa Kata ya Kibingo wakipewa Salaamu za pole. Salaamu hizi za pole zilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu Shaban Lissu alipokuwa akitoa salaamu za rambirambi kwa familia zilizofiwa na watoto wanne kwa ajali ya Radi katika kijiji cha Kihinda hivi karibuni. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilichangia kiasi cha Sh. 200,000 kwa kila mtoto aliyefariki. Aidha Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu alichangia Sh. 100,000 kwa kila mtoto aliyefariki katika ajali hiyo akiwakilishwa na Mkuu huyo wa Wilaya na kufanya kiasi tolewa kuwa Sh. 300,000 kwa kila mtoto aliyefariki na kufanya jumla ya Sh. 1,200,000 kutolewa kama rambirambi kwenye maafa hayo yaliyotokea. "Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Ameni"
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved