Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia Sheria mkononi kwani ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Ameyasema hayo tarehe 21 Oktoba 2025 katika kijiji cha Kibingo kata ya Kibingo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Wilaya ya Kyerwa.
Aidha Mhe. Msofe amewataka wananchi kujitokeza katika zoezi la kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 ili waweze kuwachagua viongozi wanaowapenda na watakao waletea maendeleo.
Vile vile Mhe. Msofe amewataka wananchi waendelee kulinda na kudumisha amani hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved