Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe ametembelea Kata ya Iteera kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi zinazowakabili katika mazingira yao na kuwataka wajitokeze kwa wingi kujiadikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza tarehe 5 Agosti 2024.
Ukesefu wa maji safi na salama, barabara mbovu, kutofikiwa na umeme kwa baadhi ya Vitongoji, kutokuwa na Vitambulisho vya taifa, migogoro ya ardhi na kifamilia ni miongoni mwa kero zilizojitokeza na kutolewa ufafanuzi na wataalam walioambatana na Mkuu wa Wilaya katika ziara hiyo.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved