MKUU wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amezindua zoezi la kugawa kasiki za kutunza fedha na nyaraka za vikundi vya huduma ndogo za fedha kwa wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-TASAF katika Kata ya Nyakatuntu Wilaya ya Kyerwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa amewataka viongozi wa vikundi hivyo kuwa waadilifu na kutunza amana ya vikundi ili viweze kujiwekea akiba ya kutosha na viweze kuimarika na kuwanufaisha wanufaika hao ili waweze kujikwamua na umaskini.
“Kama viongozi sio waadilifu watatuingiza kwenye majanga, kwa hiyo viongozi mmepewa dhamana ya kulinda amana hiyo ya kikundi, kwa hiyo muonyeshe kweli nyinyi ni viongozi na muwe waadilifu, isije ikatokea migogoro mkafungue mkatoa hela na kukimbia na visanduku.” Amesema Mhe. Msofe.
Awali mratibu wa TASAF Wilaya ya Kyerwa Bw. Emmanuel Lyanga amesema Wilaya ya Kyerwa inavikundi 363 ambavyo vimejiwekea akiba ya fedha ambayo mpaka sasa Kiwilaya ipo akiba ya Tsh 143,071,500 ambavyo vikundi vimejiwekea akiba na wanufaika wanaendelea kukopeshana.
Kwa upande wake Mchumi wa Kikundi cha Tupendane Bi. Samera George ameishukuru Serikali kwa kuwagawia kasiki hizo ambapo awali walikuwa wanatumia njia ambazo sio salama kwa utunzaji wa fedha na kumbukumbu za vikundi vyao ambavyo ilipelekea kupotea kwa fedha na kumbukumbu za vikundi.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved