Katika mchezo wa kusisimua uliochezwa kwenye Uwanja wa Isingiro leo tarehe 20, Septemba 2025, timu ya Nyaruzumbura imeibuka mshidi baada ya kushinda penati 4‑3 dhidi ya timu ya Rwabwere baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana.
Kwa ushindi huo, timu ya Nyaruzumbura imejipatia kombe na kitita cha pesa taslimu shilingi Milioni mbili, na Mshindi wa Pili, Rwabwere imejinyakulia Milioni moja huku Timu ya Isingiro ikishika nafasi ya tatu na kujinyakulia Shilingi laki tano.
Mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyerwa walijitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo wa kukatana na shoka wakiongozwa na Mgeni Rasmi wa Mchezo huo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Zaituni Msofe.
Akizungumza baada ya Mchezo huo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa amesema Serikali itaendelea kuunga mkono wanaoanzisha ligi katika maeneo yao kwa lengo la kukuza michezo na kutoa fursa kwa vijana.
"Nawapongeza Abdulmajid Nsekela Foundation kwa kudhamini mashindano haya ya ligi ya 'Nsekela Cup' ambayo yanatoa nafsi ya kukuza vipaji vya vijana wa kwetu ndani ya Wilaya ya Kyerwa," amesema Mhe. Msofe.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved