Wananchi wa kata ya Rutunguru,Wilaya ya Kyerwa wameanza kukusanya vifaa vya asili kama mawe, na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya kata yao. Hii imekuja mara baada ya wakazi wa Rutunguru kuchoshwa na adha ya kufuata huduma za afya umbali mrefu.
Rutunguru ni moja ya kata chache Wilayani hapa ambazo toka Uhuru hazijawahi kuwa na Zahanati.Kwa kushirikiana na wenyeviti wa vijiji na vitongoji walioapishwa hivi karibuni baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019,wameamua kuendeleza ujenzi wa zahanati ya Rwenshenshe ambayo kwa muda mrefu ilipangwa kujengwa lakini ikakwama.
Kwa muda mrefu wakazi wa Rutunguru wamekuwa wakitegemea Zahanati ya Kaisho na Hospitali ya Mtakatifu Thomasi-Isingiro kwa ajili ya kupata huduma za afya.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved