Mtu mmoja mwanamke mwenye umri wa miaka 25 akututwa na maambukizi ya UKIMWI, kati ya watu 77 waliopima virusi hivyo katika siku ya maadhimisho ya UKIMWI Wilayani Kyerwa.Upimaji huo umefanyika kwa jumla ya watu 77, wakiume wakiwa ni 44 na wakike 33.
Akisoma risala ya maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa wenye ujumbe unaosema “mshikamano wa kimataifa tuwajibike kwa pamoja” ndugu Philibert Binamungu alisema kwamba ufuasi sahihi wa tiba itolewayo kwa WAVIU(Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI) ni moja ya misingi ya kuimarisha afya, utu na ari ya kuishi maisha bora bila unyanyapaa kwa wanaoishi na VVU katika jamii.
Takwimu za hali ya maambukizi kwa Wilaya ya Kyerwa. Mwaka 2019 hali ya maambukizi ya UKIMWI ilikuwa kuwa kama ifuatavyo:- Waliopimwa ni 64,078, kati ya hao wanaume ni 32,390 na wanawake waliopima ni 32,214. Waliogundulika kuwa na maambukizi ni 3,182 sawa na 4.9%, kati ya hao 1,440 ni wanaume na 1,742 ni wanawake. Kwa mwaka 2020 upimaji umefanyika na waliopima ni kama ufuatavyo:- Jumla ya waliopima VVU ni 14,723, kati ya hao wanaume ni 6928, na wanawake ni 7895 . Waliogundulika kuwa na maambukizi ya VVU ni 1,948 sawa na 13.2%. Takwimu hizi za miaka miwili zinaonesha kuwapo kwa ongezeko la maambukizi ya VVU kwa 8.3% ikilinganisha na mwaka 2020. Hii inatokana na ukweli kuwa, mwaka huu upimaji umewafuata walengwa ambapo ni pamoja na kupima wenza wa waishio na VVU kwa kufuata mnyororo( Index testing) na kuwaibua.
Maadhimisho hayo yalifanyika katika kijiji cha Kigorogoro kata ya Kibale hapa Wilaya ya Kyerwa, na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi ndugu Scalion Boniphase Kagaruki ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kibale.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved