Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi ameridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Kyerwa.
Ndugu Ussi baada ya kutembelea, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya Msingi katika Miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 tarehe 11 Septemba 2025, amesema Wilaya ya Kyerwa imetekeleza miradi kwa ufanisi mkubwa na ameridhishwa na utekelezwaji huo.
Miradi hiyo ni; Kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Barabara ya Mkwenda-Mabira yenye urefu wa 1KM na Mradi wa Maji Mabira, Kutembelea Kitalu cha Miche ya Miti cha Kadres-Kitwe, Kuzindua Tawi la Benki ya CRDB la Nyakatuntu Kyerwa.
Miradi mingine ni kutembelea Mradi wa Vijana Muungano Kyerwa wanaojishughulisha na Ufyatuaji wa matofali ya Block ,kuweka jiwe la msingi katika Wodi ya Wazazi- Zahanati ya Rukuraijo na Kufungua Mradi wa Vyumba Vitatu vya Madarasa na Ofisi moja yaWalimu katika Shule Msingi Muhurile katika kata ya Nkwenda.
Miradi yote imekubaliwa na Mwenge wa Uhuru na kuipongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo inayotekelewa katika Wilaya Kyerwa.
Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa urefu wa 75Km na unataraijwa kukabidhiwa katika Wilaya ya Karagwe tarehe 12 Septemba 2025.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025 ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu".
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved