Wajumbe Baraza la Wafanyakazi Wilaya ya Kyerwa wamefanya kikao maalum cha baraza leo tarehe 20 Februari 2024 ili kupitia na kujadili rasimu ya mpango wa makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Akiongoza kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mwl. Stephano Ndabazi amewashukuru wajumbe kwa michango yao ambayo ilijikita kujadili maswala ya maslahi ya watumishi wa umma ikiwemo kulipa madeni ya watumishi, kuboresha mazingira ya wafanyakazi, kuboresha zawadi za wafanyakazi bora ikiwa ni pamoja na kujali watumishi wenye mahitaji maalum, pamoja na kuzingatia uwiano jinsia.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved