Waziri wa nchi, ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jaffo amesikitishwa na maendeleo hafifu ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani hapa, mheshimiwa Jaffo amemlaumu mkandarasi SUMA JK kwa kuzembea kukamilisha mkataba wa ujenzi ambao ulianza mnamo tarehe 30 Juni, 2018 na ulitakiwa kukamilika tarehe 6 Disemba, 2020 ukiwa na thamani ya shilingi bilioni 1.7 hadi walipoishia ujenzi.
Mheshimiwa Jaffo alibainisha mapungufu ya Mkandarasi SUMA JK, kuwa wamekuwa na tabia ya kutelekeza miradi wanayoisimamia iliyopo pembezoni mwa nchi, kwa kigezo kuwa macho ya Serikali yapo mbali kuikagua.
“SUMA JK tunzeni heshima yenu , hamuwezi kusimamisha kazi kwa kusubilia certificate ya milioni 100”, alisisitiza mheshimiwa Jaffo. Mheshimiwa Waziri, ameagiza Jengo hilo lianze kujengwa kupitia mfumo wa False Akaunti ambapo Mkurugenzi Mtendaji kupitia Mhandisi wa Halmashauri.
Pamoja na ziara hiyo, mheshimiwa Jaffo alikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ambapo alifurahishwa na maendeleo ya hospitali hiyo na kuahidi kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na ukamilishaji wa miundombinu.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved