Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mheshimiwa Rashid Mwaimu, ameongoza zoezi la ugawaji wa vifaa vya ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa kwa shule 5 za sekondari Wilayani hapa.
Halfa hiyo iliyofanyika katika kata ya Rutunguru ilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Diocles Ngaiza, Kamati ya Ulinzi na Usalama,Wakuu wa Idara, Kamati ya Maendeleo ya
Kata , na jamii .Jumla ya shule 5 mpya za sekondari,kutoka kata za Nyaruzumbura, Rutunguru, Bugara, Kakanja, na Mabira zilipatiwa vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na mabati 580, saruji mifuko1030,madirisha 84, milango 24, misumali kilogramu 90.Jumla ya gharama za vifaa hivi ni shilingi 68,668,000/=.
Ujenzi wa shule ya Sekondari Nyazumbura unaendelea ambapo vyumba 5 vya madarasa vimefikia hatua ya umaliziaji, na chumba 1 cha darasa kipo hatua ya msingi. Pia ujenzi wa matundu 10 ya vyoo vya wanafunzi upo katika hatua ya umaliziaji, wakati matundu 2 ya vyoo vya walimu yapo katika hatua ya kuchimba shimo.
Ujenzi wa shule ya Sekondari Rutunguru unaendelea ambapo vyumba 2 vya madarasa vipo katika hatua ya uwezekaji, na chumba 1 cha darasa kipo katika hatua ya msingi. Aidha matundu 8 ya vyoo vya wanafunzi na matundu 2 ya vyoo vya walimu umefikia hatua ya umaliziaji.
Ujenzi wa shule ya sekondari ya Bugara vyumba 3 vya madarasa vipo katika hatua ya msingi.Ujenzi wa shuleya sekondari Kakanja vyumba 3 vya madarasa vipo katika hatua ya uezekaji,pia ujenzi wa matundu 10 ya vyoo vya wanafunzi upo hatua ya uezekaji. Aidha, ujenzi wa shule ya sekondari Mabira ujenzi unaoendelea ni chumba 1 cha wanafunzi wa kidato cha tano ambapo hatua iliyofikiwa ni umaliziaji.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved