Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Zaituni Msofe amewaongoza Wananchi na Watumishi wa Wilaya ya Kyerwa kushiriki zoezi la kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ikiwa ni miongoni mwa shughuli zinazofanyika kuelekea siku ya Mazimgira duniani.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Kimkoa katika Kata ya Mabira Wilaya ya Kyerwa Juni 05, 2025 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa anatarijiwa kuwa Mgeni Rasmi.
Mkuu wa Wilaya amesema Wanakyerwa tukiamua kufanya usafi, Kyerwa itakuwa safi muda wote na kuwapongeza wanaofanya usafi katika maeneo yao na wale waliojitokeza kushiriki katika zoezi hilo.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mwaka huu ni, "Mazingira Yetu na Tanzania IjayoTuwajibike Sasa, Dhibiti Matumizi ya Plastiki ".
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved