Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa,mheshimiwa Rashid Mwaimu ameagiza idara ya Maji kusimamia kikamilifu miradi ya maji inayotekelezwa hapa Wilayani.Mheshimiwa Mwaimu ameagiza hayo alipokuwa katika sherehe ya kilele cha wiki ya maji kiwilaya iliyofanyikakatika kata ya Kakanja,hivi karibuni.
Akikagua na kuzindua mradi huo wa maporomoko(gravity),mheshimiwa Mwaimu alimuagiza Mkurugenzi mtendaji,kuhakikisha miradi yote ya maji iliyopo Wilayani, lakini inasimamiwa na Wilaya ya Karagwe utaratibu ufanyike ndani ya mwezi mmoja,irudishwe Kyerwa kwa ajili ya usimamizi wa karibu.Aidha,mheshimiwa Mwaimu alitunuku cheti cha usajili kwa kikundi cha watumia maji NYARWEKA.
Mradi huu ,unahudumia kata mbili za Kakanja na Kikukuru,ambapo unavituo vya kuchotea maji(gati) 14 ambazo zote zipo katika hali nzuri na zinatumika.Aidha kauli mbiu ya maadhimisho mwaka huu ni "Hakuna atakayeachwa,kuongeza kasi ya ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wote katika Dunia inayobadilika kitabia ya nchi".
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved