Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, ndugu Charles Francis Kabeho amewaasa Vijana wa Wilaya ya Kyerwa kuchangamkia fursa za mikopo kwa Vijana na wanawake inayotolewa na Halmashauri.Ndugu Kibeho ameyasema hayo alipokuwa akikagua vikundi vya Vijana na wanawake wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge katika kiwanja cha mpira wa miguu Isingiro hivi karibuni.
"Vijana wa kikundi hiki cha umoja wa vijana SACCOS Ltd nawapongeza kwa hatua hii mliyo ifikia, nawahimiza na wale walio nje badala ya kulalamika maisha magumu mtaani,wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo" alisisitiza ndugu Kobelo.SACCOS hii imepatiwa jumla ya shilingi 17,000,000.00 ambapo kupitia wao, vikundi wanachama vinne (4) vimekopeshwa mashine nne (4) za kukoboa kahawa na kikundi cha Umoja wa ufundi stadi Isingiro (UVUSI) kwa mtizamo wa kuendeleza viwanda na kuinua uchumi wa nchi.
Aidha,Halmashauri imetoa jumla ya shilingi 8,000,000 kwa vikundi vya wanawake.Vikundi vilivyonufaika na mkopo huu ni vikundi 2 vya wanawake vya WAPENDANAO Tsh 4,000,000 na MAENDELEO Tsh 4,000,000.Hii inamaanisha jumla ya walengwa 193 wamanufaika na mikopo ya riba nafuu ili wajikwamue kiuchumina kuongeza kipato katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved