Shirika la chakula na Kilimo Duniani(FAO) lazindua mradi mdogo (Microproject) Wilayani Kyerwa tarehe 29 Septemba ,2017.Lengo la mradi huu ni kuweza kuinua kipato cha mwananchi kupitia miradi midogo midogo ya kilimo na mifugo kwa njia ya vikundi.Aidha Wilaya imeunda vikundi nane(8) vya kilimo na ufugaji ikiwa vitano(5) ni vya wafugaji na vitatu93) vya wakulima katika kata za Songambele,Iteera,Kamuli,Mabira,Rukulaijo,na Rutunguru.Vikundi vya kilimo vipo katika kata za Rukulaijo na Mabira na vya ufugaji vipo katika kata za Songambele,Kamuli,Rutunguru,na Iteera.
Vikundi hivi vitajikita katika kilimo katika kilimo cha migomba kwa kutumia mbegu zilizooteshwa maabara(Tissue Culture),kilimo cha mihogo(Cassava cuttings) na ufugaji wa kuku na nguruwe.Mradi huu wenye thamani ya shilingi milioni arobaini na nne ,laki tano na elfu hamsini(TZs 44,558,000) umezinduliwa na Mheshimiwa Col(Mstaafu) Shabani I.Lissu ,Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved