Serikali, kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania( TIE) leo tarehe 12 machi, 2020 imekabidhi jumla ya vitabu 25,752 kwa shule 21 za sekondari na shule 97 za msingi Wilayani Kyerwa.Akikabidhi vitabu hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Shadrack M. Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mheshimiwa Rashid Mohamed Mwaimu ameishukuru Serikali kwa msaada huo, na kuwataka walimu wavitumie vizuri vitabu hivyo ili iwe chachu ya kuongeza maarifa na ufaulu kwa watoto wetu.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amesisitiza hata wafumbia macho wazazi/walezi wote wanaowakwamisha wanafunzi waliofaulu kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka 2020 kutokwenda shuleni.Hii ni baada ya Wilaya ya Kyerwa kuwa na takwimu za kukithiri kwa vitendo vya utoro wa wanafunzi shuleni.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved